*******
Serikali imewataka Wamiliki
wa nembo nchini kuhakikisha wanafuatilia bidhaa zao sokoni na kutoa taarifa
katika Tume ya ushindani (FCC) pale wanapo baini uwepo wa bidhaa zinazoiga
alama za bidhaa zao kwa maana ya bidhaa ya bandia.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Viwanda
na Bishara, Exaud Kigahe wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
katika Kongamano la maadhimisho ya kuthibiti bidhaa bandia Duniani.
Aidha ameiomba Fcc kushirikiana na wamiliki wa
nembo na mamlaka nyingine za serikali katika kuimarisha udhibiti wa biashara
haramu za bidhaa bandia na kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuwa na imani ya
kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani FCC
William Erio amesema kuwa licha ya elimu kutolewa kwa wananchi juu ya utambuzi
wa bidhaa bandia bado kuna haja ya kuendelea kuzungumza na wafanyabiashara
umuhimu wa kuweka alama au nembo katika bidhaa zao.
Post a Comment