Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ,inatarajia kufanya kambi maalum ya matibabu kwa siku saba bure katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ili kupeleka huduma karibu na wananchi.
JKCI itashirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Namtumbo kufanya matibabu hayo ambapo hadi sasa Hospitali hiyo imefanya huduma za tiba mkoba ijulikanayo kama Dk Samia Suluhu Outreach Service kwa mikoa 16 huku wananchi 16,000 walijitokeza kupima afya zao na karibu asilimia 25 walikutwa na shikizo la juu la damu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa JKCI,Dk Peter Kisenge amesema kambi hiyo itaanza Julai 8 hadi 13,2024 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni katika kituo cha afya Lusewa na Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
"Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepuka magonjwa ya moyo n yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Hadi sasa JKCI imefanya huduma za tiba mkoba ijulikanayo kama Dk Samia Suluhu Outreach Service kwa mikoa 16 ambapo wananchi 16,000 walijitokeza kupima afya zao huku asilimia 25 walikutwa na shikizo la juu la damu.
Amesema watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa y kuja kutibiwa JKCI.
Post a Comment