JWTZ KUTOA MATIBABU BURE.

********

Timothy Marko

KATIKA kuadhimisha Miaka  (60),ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jeshi hilo limesema litafanya Zoezi maalumu la Upimaji wa Magonjwa ikiwemo VVU ,Kisukari, Saratani ya matiti pamoja na Tezi dume.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Jeshi Hilo jijini Dar es salaam Msemaji wa Jeshi Hilo Luteni Gaudentius Ilonda amesema Huduma hiyo ya Matibabu ya Bure inayotarajiwa kufanyika Septemba 1,2024 katika Kanda  za kijeshi za  mikoa ya Arusha,Mwanza,Mbeya,Tabora na Zanzibar  pamoja na vituo vya Mbagala Zakiemu,Songea , Pemba Zanzibar na Pwani eneo la Mapinga.

"Zoezi la Kijeshi litafanyika Julai 29,2024 na litahitimishwa Agosti 11,2024",alisema Msemaji Luteni Kanali Ilonda.

Kanali Ilonda alisema maadhimisho hayo yataendana sambamba na kusherehesha pamoja na mashindano ya kuenzi Utamaduni wa Tanzania ili kukuza utamaduni huo.

Hata hivyo alibainisha kuwa meli ya matibabu inatarajiwa kuingia nchini  Julai 16,2024 katika bandari ya Dar es Salaam.    

Aidha,ameleza kuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi Hilo ni Miaka 60 ya JWTZ Umoja,nidhamu,utii na uhodari ni msingi wa Jeshi letu katika kudumisha amani.

 

0/Post a Comment/Comments