Kituo Cha Sheria na haki za binadamu-LHRC kimewataka wananchi nchini a wenye sifa wajitokeze kwa wingi katika vituo vya uandikishaji ili kupata fursa ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimae kuwawezesha kuchagua viongozi wawatakao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt Anna Henga ambapo amesema LHRC kama taasisi iliyopewa ithibati na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya kutoa elimu ya mpiga kura katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wanatumia nafasi hiyo ya kuwaomba watanzania wenye sifa kama zilivyoanishwa katika Ibara ya 5 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, kujitokeza kwa wingi katika vituo vya uandikishaji ili kupata fursa ya kujiandikisha.
Post a Comment