Na Sixmund Begashe - Dodoma
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) Bw. Bernard Marcelline amekutana uongozi na wanamichezo wa Club ya Wizara hiyo kwa lengo la kupata uwelewa wa pamoja wa namna ya kuboresha club hiyo ya michezo kwa maslai mapana ya Wizara na Afya za watumishi.
Bw.Marceline amewapongeza wanamichezo wote kwa mafanikio mbalimbali waliyotokana na Club hiyo kwenye michezo mbalimbali huku akiwaasa kujipanga vyema kwenye michezo inayofuata ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka huu 2024.
Pamoja na mambo mengine wajumbe wa kikao hicho wamechagua uongozi wa muda, huku Mwenyekiti aliechaguliwa Bw. Gervas Mwashimaha ameahidi maboresho makubwa ya club hiyo na kuwa Wizara itegemee ushindi mkubwa kwenye mashindano yanayofuata.
Akifunga kikao hicho, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Abdalah Mvungi licha ya kupongeza uongozi mpya wa muda kwa kuaminiwa na wajumbe, amewataka kuhakikisha wanazitendea haki nafasi zao kwa kuwaunganisha wanamichezo na uongozi wa Wizara ili Wizara iendelee kufanya vyema kwenye mashindano mbalimbali, na kuhamasisha ushiriki watumishi wote katika michezo kwa ustawi wa Wizara na Afya zao.
Majukumu ya uongozi wa muda kuwa ni kuandaa katiba ya Club na kuratibu ushiriki wa Wizara katika SHIMIWI Mwezi wa 9 Morogoro.
Aidha, uongozi huo wa muda utadumu madarakani hadi Desemba na uchaguzi kufanyika kulingana na Katiba itakayokuwa imeundwa.
Post a Comment