Na Mwandishi Wetu
Mamlaka Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA) imesema malengo waliojiwekea ifikapo 2034 matumizi ya nishati safi yakupikia kwa wananchi iwe imefikia asilimia 80.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni katika
Banda la PURA wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya 48 Biashara
Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Aidha amesema Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ya asilimia 80 itapunguza matumizi ya nishati ambayo inachafua mazingira.
Amesema kutokana na ugunduzi wa gesi unaoendelea nchini wananchi wanapaswa kutumia nishati safi yakupikia ambayo haina madhara ukilinganisha na Nishati iliyopo kwa sehemu kubwa kwa sasa.
‘Malengo yakutumia nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 mwaka 2034 lazima,tutoke kwanye matumizi ya nishati ambayo inachafua hali ya hewa kama Mkaa pamoja na kuni twende tukatumia nishati ambayo haina madhara kwa kiasi kikubwa,’alisema Mhandisi Sangweni.
Amesema kuwa wanafanya tafiti mbalimbali zakuwezesha jambo hili liwezekane kwa kuzalisha kiasi cha gesi ambacho kitaweza kuhudumia majumbani,katika magari na kwenye maeneo mengine.
Amesema mpaka sasa kuna maeneo ambayo tayari yameshagunduliwa gesi ikiwemo Mnazi Bay pamoja na Songosongo iliyopo Mtwara.
Amesema Mamlaka inaendelea na ugunduzi katika maeneo ambayo yana viashiria vya gesi ambapo imebainika ni asilimia 50 ya eneo la Tanzania.
"Maeneo yenye viashiria ya mafuta SQM 5,034,000 karibu asilimia zaidi ya 50 za eneo la Tanzania
Amesema utafiti uliofanyika SQKM 169200 huku eneo lililofanyiwa Utafiti mwingi yapo Pwani kuanzia Kaskazini kwa maana ya Tanga,Kusini na Mtwara eneo hili limeenda mbali zaidi kuingia baharini zaidi ya km 400,eneo hili tulishapata kibali Umoja wa Mataifa (UN)na tushagawa katika vitalu,kwa kuanza ukanda huu wa Pwani tutakuwa na vitalu ambavyo tutavitangaza,’alisema Mhandisi Sangweni.
Amsema kwa sasa wanatangaza maeneo mbalimbali ambayo watavutia wawekezaji kwa ajili yakuja kushirikiana na taasisi pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwenye kutafuta na ikiwezekana kinachopatikana wakiwekee mkakati wa kukiendeleza.
Post a Comment