Mbunge Bonnah aibua Shangwe kwa Wakazi wa Tabata

...............

NA HERI SHAABAN (ILALA)

MBUNGE wa Jimbo la Segerea (CCM), Bonah Kamoli,  amewatangazia wakazi wa Jimbo hilo ambao kwa miaka takriban Sita wamekuwa wakisubiri kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi, waenelee kuishi kama kawaida, mpaka Serikali itakapotangaza upya kulipa fidia kupisha mradi wa Mabasi ya Mwendokasi Kasi awamu ya sita.

Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mtambani, Paul Abel, alipohojiwa sababu za kushangilia kauli hiyo, amesema kwa miaka Sita ameishi bila kukarabati nyumba  kwa namna yoyote makazi yake, wapangaji wamemkimbia na hivyo kuathiri hali yake kiuchumi lakini sasa kwa kauli ya mbunge, ana uhakika wa kurejesha uhai kwa makazi yake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya TABATA Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ,alipokuwa katika mkutano wa wananchi kuelezea utekelezaji wa Ilani na mikakati ya Serikali alisema wakazi wa BARABARA ya TABATA Segerea ambao wanatarajia kupisha upanuzi wa mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam UDART  awamu ya sita  wakazi wa maeneo hayo waendeleze maeneo yao mpaka hapo Serikali itakapotangaza tena.

"Ni kweli kuna mradi wa mabasi ya haraka unapita kata ya TABATA mtapata barabara ya kisasa kwa awamu ya sita naomba wakazi mkae katika maeneo yenu mpaka hapo Serikali itakapofika kufanya fidia kupisha upanuzi wa Barabara ya Mwendokasi kasi "alisema Bonah. 

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alisema  mipango ya Serikali katika suala la miundombinu ya Barabara wilaya ya Ilala mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP ukikamilika asilimia 80 ya kero zitakuwa zimemalizika miundombinu ya Barabara itakuwa inapitika sasa hivi Serikali imesimamia Ilani vizuri mwaka 2010 mradi wa DMDP  kulikuwa na changamoto za kisasa hivyo mradi ulikosekana  .

Mbunge Bonnah Ladslaus akizungumzia changamoto ya maji ya DAWASA alisema Waziri wa maji alifika katika jimbo hilo kutatua kero za maji na kubadirisha Watendaji wa DAWASA hivyo maji yatafika  maeneo yote.

 Akizungumzia kero za Tabata Kisiwani alisema Tabata kisiwani Changamoto yao kubwa mtaa mkubwa lakini auna shule ya Msingi kata ya Tabata ina mitaa nane mitaa. Sita ina shule Mandela na Kisiwani aina shule ya Msingi wala Sekondari.

Alipongeza Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM vizuri kwa kueleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara. 

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam kwa ushirikiano wao mkubwa na kuakikisha maendeleo yanakuwa kwa kasi jimbo la segerea 

Mbunge wa Jimbo la Segerea alianza Ziara na mikutano ya hadhara kata ya Liwiti,Kipawa ,Kimanga na TABATA katika mwendelezo wake katika kata 13 jimbo la segerea. 

0/Post a Comment/Comments