MBUNGE SHANGAZI AFURAHISHWA NA WANAKIJIJI KUJITOA KUFANYA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Rashid Shangazi akizungumza na wanakamati wa umoja wa wanakijiji wa Kijiji cha Nkelei ambao wameupa jina ‘NKELEI NA MABADILIKO’ katika kikao ambacho kimefanyikia jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Umoja wa Nkelei na Mabadiliko Kassim Kipingu akisoma Risala na kuanisha malengo ya chama chao mbele ya  Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Rashid Shangazi katika kikao ambacho kimefanyikia jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo katika umoja huo wa ‘NKELEI NA MABADILIKO’ Rasuli Chanoga akifuatilia kwa makini kikao cha baina yao wanakamati na Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Rashid Shangazi katika kikao ambacho kimefanyikia jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wajumbe wakamati ya Umoja wa ‘NKELEI NA MABADILIKO’ ambao wamehudhuria kwenye Kikao hicho kwa ajili ya kujadili maendeleo wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Rashid Shangazi katika kikao ambacho kimefanyikia jijini Dar es salaam.

...................

NA MUSSA KHALID 

Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Rashid Shangazi ameahidi kuendelea kuungamkono jitihada za maendeleo ambazo zinafanywa na wananchi wa Nkelei katika Kata ya Rangwi ili kuodnoa changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Pia amewataka wanakijiji wa Kijiji cha Nkelei kuepukana kusikiliza maeneo ya watu wasiopenda maendeleo badala yake waendelee kupambana kusaidia kukijenga kijiji chao katika upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo ya upatikanaji wa maji,elimu,Afya na miundombinu ya barabara.

Mbunge Shangazi amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na umoja wa wanakijiji wa Kijiji cha Nkelei ambao wameupa jina ‘NKELEI NA MABADILIKO’ambao kwa juhudi zao za kuiunga mkono serikali wamefanikiwa kujenga Shule ya Sekondari pamoja na Zahanati katika ili kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho.

‘Mimi kitu ambacho ningependa niwaambie watu wanaochochea chuki za kimaendeleo tusiwape nafasi kwa sababu kama leo tungeisubiri serikali itujengee sekondari isingekuwepo lakini tumeanza na tunaiona wewe kama ulikuwa una mtoto wako anaenda shule ya mbali Nduruma sasa anakwenda karibu’amesema Mbunge Shangazi

Aidha kuhusu suala la Huduma za Afya  Mbunge huyo amesema wanamalengo ya kujenga kituo cha Afya ili kuweza kusaidia maeneo mbali ya karibu na kijiji hicho ikiwemo Mbaru,Masereka,Manolo na Rangwi nzima kwa ujumla

Mbunge huyo ameendelea kusisitiza kuwa suala la Zahanati ni la kwakwe hivyo atahakikisha mwaka huu litaisha kwa kufanyiwa usafi ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.

Kuhusu suala la umeme mpaka sasa mradi mradi umewafikia baadhi ya ya vitongoji katika kijiji hicho huku maeneo ya Dule,Kweibuva,Mtimule ,Dukani yakiwa hajafikiwa hivyo Mbunge amechukua majina ya maeneo hayo na kuhakikisha anaviweka kwenye mpango wa utekelezaji.

Vilevile katika suala la miundombinu ya Barabara,Mbunge Shangazi ameahidi katika bajeti ya mwaka huu atahakikisha barabara ya Mbaru-Nkelei inatengenezwa.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Umoja wa Nkelei na Mabadiliko Kassim Kipingu amempongeza Mbunge huyo kwa kuendelea kuwaunga mkono katika kila mipango yao ya kufanya maendeleo.

‘Kwa sababu chama hiki ni miongoni mwa sehemu ya uzalishaji wa maendeleo ambayo pia na wewe unaisimamia katika jimbo lako na wewe kama sehemu ya familia hili pio liposehemu yako namomba na hili uweze kuliweka katika akili yako’amesema Kipingu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo katika umoja huo Rasul Chanoga amesema wataendelea kuhamasisha wanakijiji kushiriki katika juhudi za maendeleo ili kuiunga mkono serikali katika utatuzi wa changamoto mbalimbali kwenye kijiji chao

Amemshukuru Mbunge kwa kuendelea kuwaunga mkono katika juhudi zao za kimaendeleo kwani amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa sekondari pamoja na Zahanati.

Haya hivyo Mbunge huyo amewashauri kuendelea kuwa na malengo hayo waliyojiwekea Ili Umoja huo uendelee kudumu wakati wote.

0/Post a Comment/Comments