MKURUGENZI WA TAEC AFANYA ZIARA OCEAN ROAD


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage alipofanya ziara yake kwenye Taasisi hiyo .

***************

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed, leo amefanya ziara katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Prof. Najat amepata fursa ya kujionea uwekezaji Mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita zikiwemo Mashine za X-ray, CT Scan, MRI, pia kuna Mashine za uchunguzi za nyuklia, Gama Camera n.k.

Prof. Najat pia ametembelea Mashine ya PET-CT/Scan pamoja na kiwanda Cha Cyclotrone na Mashine za Tiba Mionzi za kisasa za Linac.

Aidha Prof. Najat amesema kuwa amejifunza kwamba Taasisi ya Saratani Ocean Road ni mfano nzuri katika matumizi ya sayansi ya mionzi kwa kuwa Taasisi hiyo imepiga hatua kutoka matumizi ya kikale na kwenda matumizi ya kisasa ya mionzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema ziara ya Prof. Najat Kassim Mohammed imetokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya TAEC na ORCI kwa muda mrefu.

Dkt. Mwaiselage amesisitiza kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road inatoa huduma za kisasa na za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya saratani ambazo baadhi ya nchi za jirani huwezi kuzipata.





Picha Mbalimbali katika ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed   katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed,  na baadhi ya watumishi wa Ocean Road alipofanya ziara yake kwenye Taasisi hiyo.

 

0/Post a Comment/Comments