*******
Mwanaume mmoja wa Ujerumani aliye na umri wa miaka 60, huenda akawa mtu wa saba kupona Virusi vya Ukimwi baada ya kupandikizwa Uloto.
Mjerumani huyo, ambaye ametaka kutotajwa
majina, amepachikwa jina la "mgonjwa anayefuata wa Berlin".
Daktari mtafiti katika hospitali ya chuo kikuu
cha Charite cha Berlin Christian Gaebler, amesema timu yao haiwezi kuthibitisha
kwa uhakika ikiwa virusi vya VVU vimetokomezwa kabisa kwa mgonjwa huyo.
Mgonjwa wa awali wa Berlin, Timothy Ray Brown,
alikuwa mtu wa kwanza kutangazwa kuponywa VVU mnamo mwaka 2008.
Hata hivyo, Brown alikufa kutokana na saratani
mwaka 2020.
Mwanaume huyo aligunduliwa mara ya kwanza kuwa
na maambukizi ya VVU mwaka 2009.
Mafanikio ya upandikizaji Seli Shina kwa watu
wenye VVU, yametangazwa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa 25 wa kimataifa wa
UKIMWI katika mji wa Munich mapema wiki ijayo.
Cc DwKiswahili
Post a Comment