PURA KUONGEZA WAWEKEZAJI


 ********

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli nchini(PURA) imebainisha kuwa itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye maeneo ambayo yako wazi ili  kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani .

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi PURA, Halfani Halfani,ameyasema hayo mapema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea . 

Aidha,Halfani, amesema PURA ina majukumu ya kusimamia na kudhibiti shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa hawana wawekezaji wa kutosha hivyo PURA itahakikisha  inaongeza wawekezaji hao katika maeneo ambayo yapo wazi.

Hata hivyo,Halfani, amesema jukumu lingine la PURA ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Petroli juu ya mambo yanayohusu mkondo wa juu wa Petroli nchini.

"PURA tunajukumu la kusimamia shughuli zote za mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kwa ajili ya soko la nje ya nchi."amesema  Hafani

Kadhalika,mwenyekiti huy,ameyataja mafanikio yaliyopatikana kwenye gesi asilia kuwa ni pamoja na kuchangia kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, kupitia majumbani, na kwenye magari.

Amesema watanzania zaidi ya 1,428 wamepata ajira za kudumu na za muda katika miradi ya ufatiliaji wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini 

"Kuanzishwa Kwa kazidata ya watoa huduma wa kitanzania ambapo Kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa". amesema Halfani na kuongeza sh. Billioni 173 zimeokolewa kupitia kaguzi za mikataba ya uzalishaji na ugawaji wa mapato

Amezumgumzia maonesho haya kwa kusema awali yalikuwa kama gulio lakini kwa sasa yameboreshwa na kuwa na hadhi .

"Naipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kusimamia na kuyawezesha maonesho haya na kuwa na hadhi ya kimataifa ".amesema 

Hata hivyo amewataka wawekezaji wenye uwezo kuwekeza kwa kuwa Tanzania ni sehemu salama pa biashara na uwekezaji.


0/Post a Comment/Comments