Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kulia akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 12,2024 jijini Dar es Salaam juu ya tuhuma za udanganyifu kwenye mitihani ya vyuo vikuu nchini.********
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
amesema hatoingilia mamlaka za Vyuo Vikuu zinapochukua hatua mbalimbali za
kinidhamu katika udanganyifu wa mitihani
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 12, 2024 jijini Dar es Salaam
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu taarifa zinazotolewa na baadhi
ya vyombo vya Habari juu ya udanganyifu katika vyuo vikuu hasa kwenye masuala
ya mitihani ambapo amesisitiza kuwa katika vyuo vikuu mtu akifanya udanganyafu
katika mtihani adhabu ni kufukuzwa chuo.
‘’Kila tunaposikia tuhuma tunachukulia kama jambo zito,
kulikuwa na dalili kama hizo katika mitihani ya darasa la saba, kidato cha Nne
na Sita, na tulichukua hatua kali, ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata
maslahi ya baadhi ya wawekezaji katika sekta ya elimu’’ Alisema Mkenda.
Ameongeza kuwa suala la udanganyifu katika mitihani lina
madhara makubwa kwani linaondoa usawa, na kwamba Serikali inataka Wanafunzi
wanapofanya mitihani wapimwe kwa usawa na haki, isitokee mmoja anafanya mtihani
kwa udanganyifu na kufaulu wakati mwingine anatumia juhudi zake.
Amesisitiza kuwa endapo mwanafunzi atabainika kufanya vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani atatimuliwa chuoni mara moja.
Aidha amewataka kuacha kutumia baadhi ya watu wenye vyeo Serikalini kutaka kuwasaidia, nabadala yake wafuate utaratibu wa kisheria.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kulia akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 12,2024 jijini Dar es Salaam juu ya tuhuma za udanganyifu kwenye mitihani ya vyuo vikuu nchini, Kushoto ni Katibu Mkuu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Charles Kihampa
Post a Comment