TIRDO YATAKIWA KUBAINI VIWANDA NCHINI

Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) limetakiwa kuhakikisha kabla ya mwezi wa tano mwakani wanatembelea mikoa yote 26 kubainisha nchi ina viwanda vingapi vilivyojengwa na vinavyofanya kazi. 

Maagizo hayo yametolewa mapema leo na  Waziri wa viwanda Dkt. Selemani Jafo wakati alipofanya ziara na kukagua namna shirika hilo linavyofanya  kazi.

Jafo amewapongeza TIRDO kwa kuwa na mfumo wa digitali wa kutambua viwanda nchini ambao mpaka sasa umeshafanya kazi katika mikoa mitano ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Arusha ja Kilimanjaro huku akiahidi hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu kuuzindua rasmi mfumo huo.

Aidha amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kutembelea viwanda na siyo kukaa ofisini 

“Wekeni utaratibu wa jinsi gani tutafanya mwaka huu utakapoisha tuwe tumekamilisha tupate idadi ya viwanda vyote nchini Tanzania watu waende site wasikae ofisini mgawane katika mikoa mbalimbali chini ya kkurugenzi wa idara ya TEHAMA” Amesema Waziri Jafo.






 

0/Post a Comment/Comments