*****
Timothy Marko
SHIRIKA la Reli Nchini (TRC)limesema kuwa linatarajia kujenga Hoteli Za Wasafiri waNyota Tano.
Akizungumza katika Ziara maaluum iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa Mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika Hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Hilo, Masanja kadogosa amesema Uamuzi huo umetokana na Uzoefu walioupata Nchini China juu ya Uendeshaji wa sekta ya Reli.
"Tumejifunza kwa Wenzetu katika Uzalishaji wa vyanzo vya Mapato unatokana Reli ambapo nchi ya china imeweza kuwalipa Mishahara pasipo kutegemea Serikalikuu"alisema Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja kadogosa.
Kadogosa Aliongeza kuwa Wazo lakujenga Reli na usafiri wa Reli umetokana na Maono ya Baba wataifa Hayati Mwalimu Julia's Kambarage Nyerere.


Post a Comment