TUME, WIZARA ZAKUTANA

 


***********
 Wizara ya Fedha kama Wizara muhimu katika maendeleo ya Taifa na ufanikishaji wa Maazimio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo  Nchini, imekutana na Kamati  ya usimamizi wa Dira. Wajumbe wa Tume ya Mipango na Timu ya kitaalamu na uandishi wa dira ya Maendelo 2050 ,  kuweza kupata picha kamili ya walipotoka na wanapokwenda

Mkutano huo uliongozwa na Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba pamoja Ndugu Laurence Mafuru ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kujadili mipango ya maendeleo na nini kifanyike kuelekea kufikia mwisho wa ukusanyaji maoni na uandishi wa Dira 2050.

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kuratibu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Serikali inatambua kuwa, maono na maratajio ya watanzania na mbinu za kuyafikia zinatokana na watanzania wenyewe kupitia ushirikishwaji madhubuti katika maandalizi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

 Ili kuhakikisha Dira hiyo inabeba maono na matarajio ya watanzania kwa miaka 25 ijayo, ni muhimu wananchi na wadau wote wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya Dira tangu hatua za awali hadi kukamilika kwake.

 Kwa kuzingatia umuhimu huo, wananci wamaombwa kutoa maoni yao kwa kuzingatia vipengele vya dodoso. Aidha, wameombwa kuongeza maelezo na taarifa za ziada ambayo ni muhimu kuzingatiwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Taarifa watakazotoa zitatumika katika maandalizi ya Dira na hivyo unahakikishiwa usiri wa taarifa watakazozitoa..

 Nia na Malengo ya kikao hiki ni kungalia mambo Muhimu ambayo  matarajio yetu kama Nchi yaliweka na kuangalia kama yalifikiwa na kuangalia Sasa kule tunakokwenda na yale.tunayoyachukua kuendelea nayo mbele .

Mafuru alisema pia kuwa kundi hili la wataalam ni kundi la kufikiri tulikotoka na tiunakikwenda. . Lakini pia kikao hiki kinalenga Sasa kuangalia matarajio haya na mawazo ambayo tunaenda kuyakamilisha kuyakusanya kutoka kwa wananchi yanalingana na maono ya Mipango ambao tunakwenda kujiwekea. Hata Sasa tunapokwenda kuangalia maoni tunatakiwa kuwa na sura halisi ya uchumi sanjari na Malengo ambayo tutataka kiyanona yakifikiwa. .

Na sisi kama tume pekee bila wizara hatuwezi kusonga mbele . Hivyo basi tumekuana ili kujadili Kwa kina na kujiwekea mkakati na Malengo ambayo si yakufikirika lakini kutekelezeka

0/Post a Comment/Comments