UCHIMBAJI WA MADINI WASIMAMISHWA KIVU


 *******

Mamlaka katika moja ya jimbo moja lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imetangaza kusimamishwa kwa shughuli zote za uchimbaji madini ili "kurejesha utaratibu" katika sekta hiyo.

Afisa Habari wa jimbo hilo la Kivu ya Kusini Danny Bashige, amesema Gavana wa jimbo hilo Jean-Jacques Purusi "anataka kudhibiti uchimbaji holela ya madini katika eneo hilo." Pasipo kutoa ufafanuziwa kina taarifa ya Gavama huyo inasema "shughuli za uchimbaji madini zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena kwa sababu ya "usumbufu unaosababishwa na waendeshaji madini.”

Pamoja na sababu hiyo nyingne sio tu kuyalinda maisha ya watu, lakini pia ufuatiliaji wa uzalishaji wa madini katika maeneo hayo.

 Kutokana na taarifa hiyo makampuni ya uchimbaji madini, wafanyabiashara na washirika wengine wamepewa masaa 72 kuondoka katika maene ya machimbo.

ccDwkiwahili

0/Post a Comment/Comments