Na Nitomth Marko.............
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa, umewataka vijana wote Nchini kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni inayolenga i kujadili kwa pamoja fursa mbalimbali zilizotengenezwa na zinazotengenezwa kwa Vijana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akitoa taarifa hiyo leo Julai 4, 2024 jijini Dar es salaam, katibu Mkuu wa UVCCM Joketi Mwegelo amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Julai 6, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Amesema Kampeni hiyo itaambatana na kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa hususani kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura pamoja na kugombea katika nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu.
" Kampeni hii kubwa ina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki shughuli za kisiasa , kujiandikisha daftari la kudumu la wapiga kura litakalozinduliwa Julai 25 mwaka huu mkoani Kigoma" amesema
Nakuongeza kuwa Kampeni hiyo itazinduliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Balozi Emmanel Nchimbi,hivyo vijana wote wajitokeze siku hiyo ili kufahamu fursa zilizotengenezwa chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha ameongeza kuwa vijana ni wabunifu na wenye kuleta mawazo mapya ya kuinua na kuendeleza uchumi wa Taifa letu hivyo kupitia
Post a Comment