WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA


********


Na Mwandishi wetu;-  

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo amewataka Wananchi kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kupiga vita dhidi ya ukatili wa Kijinsia ikiwemo Ubakaji na Ulawiti Watoto kwa kisingizio cha kujipatia mali au utajiri.

“Hakuna utajiri au mali zinazopatikana kwa njia ya kufanya ukatili hivyo niwasihi ndugu zangu wana Dareda na Watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii na ambayo haivunji sheria na taratibu za nchi kwani utajiri wa halali na wa amani unapatikana kwa kufanya kazi tu nasi vinginevyo” Alisema Mhe. Sillo

“Tabia hii si asili yetu na si mila na destuli ya Watanzania tunapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kupiga vita vikali vitendo hivi”Alisema Mhe. Sillo

Akizungumza Julai 7, 2024 wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Dareda katika muendelezo wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi wa Jimbo hilo amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali hususani Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kutoa taarifa mapema endapo mtu ataona viashiria vyovyote vile. 

Hatua hii inakuja kutokana na kulipotiwa kukithili kwa matukio kama hayo katika maeneo mbalimbali hapa nchini pamoja na baadhi ya Vijiji katika Jimbo hilo. 

Amesema ili kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ni muhimu Wazazi, Viongozi wa Dini, Wazee wa kimila na Wananchi kwa ujumla kushikikiana na Serikali katika kupiga vita na kufichua uovu huo ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.




 

0/Post a Comment/Comments