WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amefanya ziara ya ukaguzi katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yaliyopo eneo la Mazwi, Sumbawanga mjini, mkoani Rukwa tarehe 16 Julai 2024.
Katika ziara hiyo, Bw. Marwa Range, Meneja wa Kanda ya Sumbawanga - NFRA alieleza kuwa uwezo wa kuhifadhi nafaka za mahindi katika eneo la Mazwi ni tani 28,500 ambapo zoezi la ununuzi linaendelea katika maghala hayo.
Waziri Bashe alipata wasaha wa kukagua mizani ya digitali ambayo imeanza kutumika na kujiridhisha na shughuli ya upimaji wa nafaka unaondelea. Aidha, alielekeza mizani iongezwe ili kuharakisha zoezi la upimaji kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema leo wakati wa uzinduzi wa maghala ya NFRA katika eneo la Kanondo.
Aidha, Waziri Bashe amefurahishwa kuona Wakulima mbalimbali wakiwasilisha mazao yao kwa maghala ya Mazwi na kusisitiza kasi ya upimaji iongezwe. Vile vile, amemuelekeza Dkt. Andrew Komba, Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA kukarabati maghala hayo ili huduma kwa Wakulima zisikwame.
Post a Comment