Na lilian Ekonga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za hisani za Maendelo Bank zenye lengo kusaidia vituo viwili vya watoto kwenye Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro ambapo itasaidia watoto waliozaliwa chini ya miezi 9 pamoja na kituo cha watoto yatima cha mtoni Dikonia kilichipo Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mbio hizo zitafanyika tarehe 7.9.2024 kwenye viwanja vya farasi Jijini Dar es salaam Hayo ameyasema Mkuu wa idara ya biashara Maendeleo Bank Emanuel] Mwaya Jijini Dar es salaam leo Julai 24.2024 wakati akiongea na waandishi wa habari
Emanuel amesema watoto wengi wamekuwa wakifariki wakikosa huduma mbalimbali ikiwemo vitanda na vifaa mbalimbali .
"Katika Hospitali ya KCM zaidi ya watoto 500 wanazaliwa kila mwaka lakini uhitaji ni mkuwa kuliko vifaa vinavyohitajika na kwasababu hiyohiyo watoto wengi wamekuwa wakifariki kwa sababu ya kukosa huduma mbalimbali ikiwemo vitanda na changamoto nyingine.
"Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 25% mpaka 30 ya watoto wanaofika pale watoto karibu 150 kati ya 500 wanafariki moja ya sababu kubwa iliyotajwa ni ukosefu wa vifaa"amesema Emanuel
Kauli mbiu ya mbio hizo ni hatua ya faraja msimu wa pili.
Post a Comment