|
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mwanaasha K. Juma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati yake kufanya mazungumzo na menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation) katika ziara yao ya mafunzo kutembelea TTCL. |
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mwanaasha K. Juma (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati yake kufanya mazungumzo na menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation) katika ziara yao ya mafunzo kutembelea TTCL. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation), CPA Moremi Marwa. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation), CPA Moremi Marwa akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kufanya ziara ya kujifunza kutembelea Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mwanaasha K. Juma. |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia ziara yao ndani ya Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wajumbe wengine walioambatana katika ziara hiyo wakipata picha za kumbukumbu mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia ziara yao ndani ya Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation), CPA Moremi Marwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi kutembelea Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. |
|
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia ziara yao ndani ya Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. |
|
Mkutano huo na waandishi wa habari ukiendelea kwenye ziara ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndani ya Shirika la TTCL leo jijini Dar es Salaam. |
WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, leo wamefanya ziara yao ya kujifunza kutembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati yake kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TTCL Corporation, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mwanaasha K. Juma amesema ziara hiyo pamoja na mambo mengine ni ya kimafunzo na kujionea utendaji kazi ndani ya Shirika la TTCL.
Wajumbe hao walipata pia fursa ya Miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kutembelea Kituo cha Uangalizi na Uendeshaji wa Mtandao (NOMC) kujionea utendaji kazi.
Post a Comment