Na lilian Ekonga, Dar es salaam.
Asasi za kiraia (FCS) na baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) wameingia hubia wa miaka mitatu kushirikiana kulinda haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania wenye lengo la kuhakikisha haki na uwajibikaji katika kutoa huduma kwa watumiaji na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa.
Hubia huo unachangia maendeleo ya masoko na ukuaji wa biashara zinazoheshimu sera za kulinda watumiaji na kuwapa wateja kipaumbele kujijengea hadhi na kuziweka nafasi nzuri kiushindani
Hayo ameyasema Justice Rutenge Mkurugenzi wa Asasi na kiraia (FCS) wakati wakisaini hobia huo Agosti 6,2024 Jijini Dar es salaam
"Kupitia mradi huu tutajenga uwezo wa asasi za kirai kuboresha uwiano kati ya sera na hatua zinazochukuliwa katika nchini, Tutategemea saut thabiti kutoka asasi za kiraia nchini tanzania katika kuwatetea watumiaji na kuleta mabadiliko chanya katika kulinda haki za watumiaji" amesema Rutenge
Aidha Justice amesema ushirikiano huo ni kielelezo cha nia thabiti ya kuwawezesha watumiaji wa huduma na bidhaa na kukuza haki zao katika soko likiwa na mlengo wa kujenga mazingira bora katika soko kwa watumiaji na huduma za mawasiliano ili wawe wenye taarifa sahihi na kulinda stahiki zao nchini.
Sambamba na hayo amesema FCS kwa miaka mingi imekuwa ikisisitiza maendeleo yaliyojikita katika kuwanufaisha wananchi na kuwaweka kipaumbele .
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TCRA CCC Marry Shao Msuya amesema huduma za mawasiliano nchini zimeongezeka kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia kwa mujibu wa takwimu za TCRA kufika June 2024 kuna kadi za simu milioni 76.6 watumiaji wa intarnet milioni 39.3 akaunti za pesa mtandao milioni 55.7 hivyo idadi hiyo itaongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kidigitali.
Mary ameongezea kwa kusema mazingira ya ukuaji huo wa sekta ya mawasiliano suala la kuwalinda watumiaji lina umuhimu mkubwa kwa kuwajengea uwezo watumiaji ili wawe na uwelewa na masuala muhimu ikiwemo haki zao ,wajibu fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ili sekta wawe washiriki wenye uelewa wa masuala ya msingi yanayohusu kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanapotumia huduma na bidhaa za mawasiliano.
"Baraza linaamini kuwa watumiaji wenye uelewa wanapitumia huduma na bidhaa za mawasiliano na kuwa na uwezo wa kuwawaajibisha watoa huduma ili kupata huduma bora zenye viwango na zinazokidhi mahitaji"amesema Msuya.
Post a Comment