HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE YAZINDUA WODI YA KUSAFISHA DAMU NA GARI LA DHARURA KWA MAMA NA MTOTO

 

...........................

NA: Issah Mohamed –Dar es salaam.

EMAIL: issahmohamedtz@gmail.com

Takwimu zimeonesha kuwa kwa mwaka 2023/24 Hospitali ya rufaa  Temeke imehudumia wagonjwa wa magonjwa yasiombukiza zaidi ya elfu 11. 1 sawa na ongezeko la asilimi 14.4 kutoka mwaka 2022/23 huku miongoni mwa sababu zilizochangia ongezeko hilo ni ulaji usiofaa ikiwemo matumizi ya chumvi, Sukari pamoja na tumbaku.

Takwimu hizo zimebainishwa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Bi Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa jengo la kutolea huduma nafuu za kusafisha damu katika hospital hiyo.

Amesema uzinduzi wa jengo hilo litasaidia kupunguza mlundikano wa wagonjwa hao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku akitumia nafasi hiyo kuwataka watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ambao umeelekezwa na wataalam wa afya ikiwemo kufanya mazoezi.

‘’Kutokana na ongezeko hili niwalekeze wananchi kufuata mtindo bora wa maisha ambao unaelekezwa na wataalam ili kuepuka kupata shinikizo la juu la damu na kisukari kinachopelekea kuathiri figo’’ Amesema Mapunda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya rufaa Mkoa Temeke Dkt Joseph Kimaro amesema katika mwaka 2023/24 wagonjwa wa magonjwa yasiombukiza takribani 74 walipoteza maisha kati ya 412 waliopata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

‘’Kwahiyo baada ya kuona changamoto hii tukaona tuanze huduma hii ili kusaidia wananchi wa Temeke, Kigamboni pamoja na Mkuranga ambao hutegemea zaidi huduma zetu’’ Ameeleza Dkt Kimaro.

Uzinduzi huo pia umehusisha gari jipya la kubebea wagonjwa, ambalo limeelekezwa kitengo cha Mama wajawazito wanaohitaji huduma za dharura pamoja na kuwahudumia watoto kwa haraka na usalama.

0/Post a Comment/Comments