**********Na mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) imeotoa angalizo juu ya uwepo wa mvua za kusuasua
zitakazotawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko usioridhisha katika
maeneo mengi.
Akizungumza na waandishi
wa habari Jijini Dar es Salaam jana Agosti 22, 2024 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Hali ya Hewa (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a amesema mvua zinatarajiwa kuanza
wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika ukanda wa ziwa Victoria na kusambaa
katika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Octoba, 2024 na
zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba ,2024
Amesema licha ya maeneo
mengi kutarajia kupata mvua za chini ya wastani pia kutakuwepo na matukio ya
vipindi vifupi vya mvua na joto kali kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Dkt. Chang'a, amesema
miongoni mwa athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na upungufu wa unyevunyevu
kwenye udongo na ongezeko la wadudu na magonjwa katika mazao.
Sambamba na hayo ametoa
wito kwa Jamii kuchukua tahadhari za utunzaji Maji hususani maeneo ya mgodini
ambapo hutumia kiasi kikubwa Cha maji kwani uwepo wa mvua za wastani na chini
ya wastani kutasababisha upungufu wa Maji.
Post a Comment