RAIS DK. SAMIA ALIPONGEZA SHIRIKA LA TTCL KUFANIKISHA TAMASHA LA KIZIMKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha pongezi Meneja Mkazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Zanzibar), Bw. Hillary Mwinyi (kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) kwa kutambua mchango wa TTCL kufanikisha shunguli mbalimbali za Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha pongezi Meneja Mkazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Zanzibar), Bw. Hillary Mwinyi (kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) kwa kutambua mchango wa TTCL kufanikisha shunguli mbalimbali za Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi cheti cha pongezi kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutokana na ushiriki wake wa kipekee katika kufanikisha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar.

Cheti hicho cha pongezi kilipokelewa na Meneja Mkazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Zanzibar), Bw. Hillary Mwinyi pamoja na Meneja Mkuu wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa  TTCL wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi, Zanzibar.

Pongezi hizo ni kutambua mchango wa Shirika la TTCL katika kuunga mkono shughuli za Tamasha la Kizimkazi ikiwa ni pamoja na kufanikisha michezo na shughuli mbalimbali za kijamii, kiutamaduni na kiuchumi wakati wa tamasha kiujumla.

Ushiriki wa TTCL katika tamasha hilo umesaidia upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia Banda la Maonesho ambalo lilitoa huduma ili kuwezesha wageni na wananchi wa eneo hilo kupata huduma bora. TTCL imeendelea kushirikiana na Serikali na jamii katika kukuza utalii, uchumi, na utamaduni wa Zanzibar.

Cheti hiki cha pongezi ni ishara ya kutambua umuhimu wa TTCL katika kuimarisha maendeleo ya jamii kidigitali na kufanikisha malengo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kwa Shule ya Sekondari ya Kusini Mjini Zanzibar baada ya kuibuka Mshindi wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya 'Samia Kizimkazi Youth Cup'. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Shirika la Mawasiliano la TTCL na wadau wengine.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni moja na laki tano pamoja na kikombe cha ushindi kwa Shule ya Sekondari ya Kusini Mjini Zanzibar baada ya kuibuka Mshindi wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya 'Samia Kizimkazi Youth Cup'. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Shirika la Mawasiliano la TTCL na wadau wengine.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni moja na laki tano pamojamna kombe kwa Shule ya Sekondari ya Kusini Mjini Zanzibar baada ya kuibuka Mshindi wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya 'Samia Kizimkazi Youth Cup'. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Shirika la Mawasiliano la TTCL na wadau wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Pango la Kasa 'Salaam' lililopo Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 24 Agosti, 2024.




0/Post a Comment/Comments