Na Richard Mrusha Dodoma
Kampuni ya mawasiliano Tigo Tanzania yaja na kampeni ya sako kwa bako kanda ya kati Dodoma
Tigo Tanzania inaendelea na kampeni ya sako kwa bako nchi nzima ambayo ina mda wa miezi miwili tangu ilivyoanzana sasaa ni kanda ya kati kwa maana ya Dodoma, Tabora,Iringa
Afisa mkuu wa Biashara kutoka kampuni ya mawasiliano Tigo Tanzania Isack NChunda amebainisha hayo leo Aug1,2024 mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za Tigo kanda ya kati Dodoma
Amesema tigo ni mtandao bora zaidi nchini Tanzania kwani umeendelea kufanya uwekezaji wa zaidi ya sh Tilion 1.
Amesema tigo ni mtandao ambao unakuwa kwa kasi Tanzania na kwa mjibu wa takwiu kutoka Mamlaka ya mawasiliano Nchini( TCRA) sasa una familia zaidi ya wateja milioni 21
Tunakupatia ofa kabambe ya sako kwa bako kila mteja pindi anapo naunua bando pia anapata dakika bure kwa kanda ya ziwa Mwanza, simiyu,Kagera ,mara, kigoma na Geita unachotakiwa kufanya ni kuchagua size yako kisha utapa ofa maalum amesema NChunda",
Ameongeza kwa kuwataka wateja wao kuendelea na promosheni ya sako kwa bako ili waendelee kufurahia mtandao bora na Bomba kila wanaponunua vifurushi
Sambamba na hilo amesema wanafurahia leo kuona Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Hasan anazindua safari ya Treni iandayo haraka (SGR) ni wakati wa wateja wao kutumia huduma ya lipa kwa Simu kutata tiketi kwani huduma hiyo ni salama.
Amesema kampuni hiyo imefanya maboresho makubwa ya mtandao na biashara kwa ujumla kwa kutumia mtandao wa Tigo kwa ajili ya kurahisisha maisha.
Amesema Tigo inashiriki maonesho ya ya wakulima na wafugaji (8 8) kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma uku akiwasii wananchi wote kutembelea banda la Tigo kupata hudumu mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Post a Comment