Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume wakati akizungumza kwenye mkutano wa mapitio ya programu za nusu mwaka kwa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na homa ya Ini (NASHCOP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) jijini Dar es Salaam

Baadhi ya washiriki katika mkutano wa mapitio ya programu za nusu mwaka kwa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na homa ya Ini (NASHCOP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) ambao umefanyika jijini Dar es salaam.
.....,...........
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa Tanzania ni moja ya nchi 30 zenye wagonjwa wengi wa Kifua Kikuu, ikiwa na makadirio ya kiwango cha maambukizi 195 kwa kila watu 100,000 huku kikubwa cha maambukizi ya VVU cha asilimia 16.4 miongoni mwa watu wenye kifua kikuu.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume wakati akizungumza kwenye mkutano wa mapitio ya programu za nusu mwaka kwa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na homa ya Ini (NASHCOP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP).
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya imeadhimia kuendelea kuzipa kipaumbele afua za Kifua Kikuu, UKIMWI, Malaria, Homa ya Ini, Magonjwa ya Ngono na Ukoma ili kukabiliana na maradhi hayo.
‘Tumepiga hatua kubwa. Kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, tumegundua na kutibu zaidi ya wagonjwa wa kifua kikuu 431,000 wakiwemo watu wazima na takribani watoto 67,000. kifua kikuu sugu dhidi ya dawa inabakia kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma, ambalo linahitaji umakini wa haraka na endelevu,” amesema Dkt. Mfaume.
Kwa upande wake, Mkuu wa Programu kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Catherine Joachim, amesema amesema kwa mujibu wa Utafiti wa Athari za VVU, Tanzania 2022-2023 unaonyesha kuwa asilimia 82.7 ya watu wanaoishi na VVU wanatambua hali zao, ambapo asil8mia 97.9 yao wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU, na 94.3% wamepata udhibiti wa virusi.
Amesema kuwa asilimia 83 ya watu wanaohisiwa kuwa na maambukizi ya UKIMWI wanatambua hali zao lakini kwa vijana ni takribani asilimia 72,watoto asilimia 68 na wanaume ni asilimia 70.
Dkt Samweli Lazaro ni Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhidhiti Malaria Wizara ya Afya amesema serikali imepiga hatua kubwa katika mapambano ya ugonjwa huo kwani mpaka sasa ni chini ya asilimia 10 kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Aidha amesema katika mwaka huu wa fedha serikali imeweza kutoa zaidi ya Bill 11 kwa ajili ya kutekeleza afua ya unyunyuziaji wa dawa zinazoua viluilui vya mazalia ya Mbu katika Halmashauri 57 ambazo zina kiwango cha juu cha maambukizi
Post a Comment