SERIKALI: SEKTA YA MADINI INACHANGIA ASILIMIA 9 GDP


********
Na Timothy Marko

SERIKALI imesema katika kipindi cha Mwaka wafedha 2023/24 sekta yamadini imeweza kuchangia pato la taifa kwa Asilimia 9 hadi kufikia Julai mwaka huu jumla shilingi 753 zimepatikana ikilinganishwa 2022/23ambapo kiasi cha shilingi bilioni 753 .

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa wizara hiyo inaendelea kufanya utafiti wamadini yaliyopo Ardhidhini hadi hivi sasa eneo lilofanyiwa utafiti limefikia Asilimia 16.

"Asilimia ya Fedha za kigeni zimetokana na Mapato katika sekta ya madini" Alisema Waziri wa Madini Anthony Mavunde. 

Waziri Mavunde aliongeza kuwa hadi kufikia 2030 serikali imelenga kufanyia utafiti wa kina kwenye Ardhi ikiwa na lengo la kubaini nikiasigani cha Eneo la Ardhi lenye rasmali madini lengo nikuhakisha Asilimia 50 inapimwa . 

Kwaupande wake Mwneyekiti wa chember ya Madini nchini Mhandisi Benjamin Mchwambaka amesema kuwa lengo la taasisi hiyo nikuhakikisha sheria na kanuni katika uwekezaji zinafuatwa. 

Mkutano wa madini utakaofanyika Agosti28/29 utatoa fursa mbalimbali za madini. 

"Mkutano huu utatoa fursa mbalimbali za kujifunza wenzetu wanafanyaje katika sekta hii" Alisema Benjamin Mchwambaka.








0/Post a Comment/Comments