TAFITI ZINAZOFANYIKA ZIWAFIKIE WANANCHI JAFO

.................,..


Na Richard Mrusha Dodoma 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Seleman Jafo ametoa wito kwa uongozi wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Kufanya tafiti nyingi na kuhakikisha tafiti hizo zinawafikia wananchi ili kuondoa changamoto zilizipo katika sekta mbali mbali hapa  nchini.

Mhe.Jafo ameyasema hayo alipotembelea banda la TIRDO katika kilele cha Maonesho ya Wakulima Wavuvi na wafugaji maarufu kama Nane Nane katika Viwanja vya Nane Nane Nzuguni-Jijini Dodoma. Mhe. Jafo amesema kuwa TIRDO ina nafasi kubwa katika kufanya utafiti na kuwafikishia wananchi. ‘’Pamoja na kuwa nimeona kazi kubwa mnayoifanya lakini nataka tafiti zenu ziwafikie wananchi wengi ili thamani ya shirika hili ijulikane kote nchini’’ aliongeza Mhe.Jafo.

Maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu 2024 yalizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa tarehe 1 Agosti 2024 na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo Mhe.Rais ameongeza siku mbili za Maonesho ili washiriki waendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Katika Maonesho ya mwaka 2024 TIRDO imeshiriki kwa kuonesha tafiti mbali mbali kama vile uzalishaji wa mafuta tete yanayotokana na mimea kama maganda ya machungwa, karafuu, mikaratusi.


Tafiti zingine ni uzalishaji wa mkaa mbadala unaotokana na pumba za mpunga, uzalishaji wa mafuta ya parachichi pamoja na kutangaza teknolojia ya matumizi bora ya nishati ambayo inalenga kupunguza gharama kwa watumiaji lakini pia kulinda mazingira.

 

0/Post a Comment/Comments