NA
MUSSA KHALID
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imebaini
mapungufu michache katika miradi 26 yenye thamani ya Shilingi Bilioni
80,289,100,506.80 na kuwashauri wahusika kuyarekebisha ili miradi ikamilike kwa
wakati na kwa thamani halisi.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkuu wa TAKUKUKU (M) Kinondoni
Elizabeth Mokiwa wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi
mitatu kuanzia Mwezi April hadi Juni mwaka huu.
Aidha
Mokiwa amesema pia katika kipindi hicho TAKUKURU imepokea jumla ya malalamiko
88 ambapo 32 yamehusu rushwa na huku yasiyohusu rushwa yakiw ani 56.
Kuhusu
malalamiko hayo amesema yasiohusu rushwa walalamikaji wengine wameshauria na
majalada kufungwa na wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko
yao huku yanayohusu rushwa majalada yakiendelea kushughulikiwa.
‘Katika
kipindi husika tumefungua mashauri mapya kumi na sita katika mahakama ya Wilaya
ya Kinondoni na Jamhuri imeshinda mashauri mawili na mashauri 31 yanaendeelea
mahakamani’.amesema Mokiwa
Naibu
Mkuu wa huyo TAKUKUKU (M) Kinondoni amesema katika uzuiaji wa Rushwa kwenye
kipindi hicho wamefuatilia miradi sita yenye thamani ya Shiling Bilioni nane
hamsini na sita laki nane sitini elfu mia sita sabini na mbili senti sitini na
saba ambapo wamebaini mapungufu machache na hivyo wamewashauri wahusika
kurekebisha mapungufu hayo.
Miradi
hiyo ni pamoja na mradi wa kituo cha Afya Kinondoni, mradi wa ujenzi wa
barabara
ya
nyota njema kunduchi, mradi wa uboreshaji wa huduma za maji safi DAWASA – Wazo,Mradi
wa Vikundi vya usafi na utunzaji wa mazingira katika Manispaa ya Kinondoni,
Ujenzi wa Boksi Kalavati eneo la stop over, katika Wilaya ya Ubungo na mradi wa
ufungaji pampu ya maji Kibamba Kisarawe katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo.
Katika
hatua nyingine Mokiwa amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
wamejipanga kuelimisha wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike
kushirikiana na Takukuru kutokomeza rushwa kuanzia sasa hadi wakati wa uchaguzi
na baada ya uchaguzi.
‘Rushwa
katika uchaguzi hupelekea kuchaguliwa kwa viongozi wasio kuwa waadailifu
watakaotumia muda wao mwingi wa uongozi kurejesha fedha zao na sio kuleta
maendeleo kwa wananchi’amesema Mokiwa
Vilevile
amesema katika mwaka 2023 hadi 2024 wametekeleza Program ya TAKUKURU Rafiki kwa
kuwafikia wananchi kwenye kata 20 na kupokea kero 61 na kuzitatua kwa uharaka
ili zisiwaathiri wananchi.
Pia
amesema kuwa wameshirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa
dini,Taasisi zisizo za kiserikali,sekta ya Afya,Nishati na Maji katika
kufikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi na kushiriki katika
maonyesho na makongamamo.
Hata hivyo Taasisi hiyo imesema itaendelea kupokea malalamiko yote yanayohusu rushwa na kuyafanyia kazi kwa uharaka ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.
Post a Comment