Na Lilian Ekonga.
Azam Media kupitia chaneli yao ya sinema zetu wamezindua tamthilia mpya ya Mzani wa Mapenzi itakayoanza kuonyeshwa Agosti 23 Mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Wasiwasi mabulambo mkuu wa kitengo cha mahudhui amesema tamthiliya hiyo itaonyeshwa katika chaneli ya sinema zetu kila ijumaa hadi jumapili saa moja usiku baada ya tamthiliya ya Toboatobo kuisha mnamo tarehe 18 Agosti 2024
“Lengo la Azam Media ni kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamani wetu huku tukisukuma sanaa yetu kimataifa hasa katkka nchi za kusimi mwa jangwa la Sahara na popote ambapo AzamTvMax inaweza kufika”
Aidha Mabulambo amesema Tamthiliya hiyo imesheheni wasaniu mahiri ja chipukizi ambao wataleta uhalisia wa maisha ya ndoa na mahusiano kwa njia ya kuvutia na ya kusisimua akiwemo Cecy, Sharin Kabwita, Irene Uwoya, Patcho Mwamba n.k
Akielezea maudhui ya tamthiliya hiyo, Mabulambo amesema inawatazama wanandoa wenye mitazamo na matamanio tofauti juu ya furaha zao, ambapo Cecy anawakilisha kundi la wale wenye kuamini kuwa ndoa ni tunu inayohitaji kulindwa huku mumewe Victor anajiridhisha kuwa mwanamume barubaru katika ndoa ni yule mwenye walau mpango wa kando katika kukidhi matamanio yake ya kibinaadamu
Aliendelea kusema kuwa Mkanganyiko huo unaipoteza taswira ya Cecy ambaye nae katika kujaribu kujibu mapigo anaangukia mikononi mwa mwanamume anayedhani kuwa ni wake pekee kumbe ni kondoo aliyejivisha ngozi ya Mbuzi.
“Sintofahamu hii na mikasa mingine ya wale wanaoamini maisha ya ubachela ndio hasa mpango mzima yanainogesha tamthiliya hii ya mzani wa mapenzi na kuwa na joto muda wote tangia episodi ya kwanza” amesema Mabulambo
Post a Comment