Makamu wa Raisi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), Aderickson Njunwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2024 katika kutoa elimu juu ya masuala ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na mkutano mkuu utakaokutanisha watu zaidi ya 150.
xxxxxxxx
Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro Tanzania ( TIArb) imeandaa mkutano utaojumuisha watu zaidi ya 150 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Mabara mengine wenye lengo la kujadili usuluhishi wa migogoro ya sekta ya Ujenzi na migogoro ya uwekezaji wa kimataifa kwa njia ya mbadala.
Akizungumza kuelekea mkutano huo, Makamu wa Raisi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), Aderickson Njunwa, amesema mkutano mkuu wa Usuluhisi wa migogoro ya Kiuchumi utakaofanyika Agost 22 na 23 Alhamisi na Ijumaa, 2024 jijini Dar es Salaam.
Aidha wiki ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kiuchumi itaanza kwa kutoa elimu kwa wananchi na jamii ijue nini taasisi hiyo inafanya katika jamii na wafanyabiashara wajue namna ya kutatua migogoro kwa njia mbadala bila kufika Mahakamani.
Kwa Upande wa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Abdallah Ganzi, amesema kuwa Mahakama ya Tanzania taasisi ya TIArb na nyingine za aina hii zipo kwaajili ya kuisaidia mahakama kutatua migogoro ya baina ya watu kwa njia mbadala.
Mkutano huo utaangazia katika changamanoto na amna bora ya utatuzi wa migogoro ya Ujenzi na Uwekazaji wa kimataifa pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala hayo.
Post a Comment