Benki ya Biashara Tanzania
(TCB) imesaini mkataba wa makubaliano na
Wakala wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi zanzibar ( ZEEA) yenye lengo
la kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo
wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani humo
Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo leo jijini Dar
es salaam Katibu mkuu ofisi ya Raisi kazi uchumi na Uwekezaji zanzibar Mariam
Saadalla, amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri
visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya
tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati
na wengine waweze kukopa .
Aidha amesema Mpango huo unakusudia kuchochea
ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda
huu wa Afrika Mashariki.
"Programu hii inakwenda kuwagusa wanawake,
vijana na walemavu na tayari yameshaletwa maombi 34 ambapo 19 ni maombi rasmi
yanayotoka kwa vikundi vya wanawake, 13 kwa vijana na 2 kutoka kwa watu wenye
ulemavu" amesema mariam
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB Adamu Mihayo amesema Mkataba huo unathibitisha dhamira yao ya kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
"Mpango huu unaendana na lengo letu la
kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi. Kwa kuyawezesha
makundi maalum, tunaziinua biashara binafsi, pamoja nakuimarisha mfumo mzima wa
uchumi na kutengeneza mazingira imara ya kiuchumi"amesema Mihayo.
Nae mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Juma Burhan
Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCb kiasi cha shilingi bilioni 1.8
ili waanze utoaji wa mikopo hiyo ambayo itarejeshwa kwa kipindi cha miaka 2.
Post a Comment