*******
Meneja usimamizi wa Kilimo kutoka TIB Bi. Monica Mzilu amesema
hayo katika kilele cha maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Jijini Dodoma kuwa,
Mikopo hiyo inatolewa chini ya Mfuko wa Kilimo ambao unatoa mikopo kwa wakulima
wakubwa, wakati na wakulima wadogo kwalengo la kuhakikisha kuwa wanakuza sekta
nzima ya kilimo na mnyororo wa thamani katika sekta hiyo
” mikopo hii inawahusu wakulima wote, wafugaji, Uvuvi lakini
pia wafanyabiashara kwenye sekta hii ya Kilimo, hivyo niwahimize wakulima
kujitokeza kutumia Mikopo hii kukuza shuguli zao” amesema
Aidha amesema, Benki hiyo ina mfuko unaotoa mikopo
inayotolewa kwa wakulima kuanzia shilingi milioni 50 hadi bilioni 2 kwa
makampuni kwa riba ya asilimia tano na vikundi vilivyosajiliwa kama saccos au
'association' kuanzia milioni 50 mpaka bilioni moja kwa riba ya asilimi nne tu
ili waweze kukopesha kwa wakulima wadogo kwa riba isiyozidi asilimia nane.
"Tunatoa mikopo
hiyo yote kwenye mnyororo wa thamani wa
kilimo yaan kuanzia mwanzo hadi
kwenye masoko ,kwa maana kwamba tunatoa mkopo kujenga maghala au kununua
vifungashio au kama mtu anataka kuchakata mazao ili kuongeza thamani ili mradi
wazo husika likidhi vigezo ."
Mbali na hilo, pia TIB Wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima kuhusu fursa zilizopo katika
benki hiyo kwenye maeneo tofauti hivyo
kuwahimiza wakulima kutembelea mabanda yao kunapokuwa na maonesho mbalimbali
mfano katika maonesho ya sabasaba na Nanenane .
Bi Mzilu pia amesema kuwa TIB imekuwa ikitoa elimu na
kuwatembelea wakulima na kuwaelimisha wafahamu wanachokitaka lakini pia wanawaelimisha
jinsi ya kutunza fedha na masuala mbalimbali ya biashara
Wakulima, Wavuvi na Wafugaji wanahimizwa kutembela ofisi za
Benki hiyo zilizopo katika kanda zote nchini, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na
Arusha
Post a Comment