NA
MUSSA KHALID
Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imewapongeza wanahabari kwa mchango wao wa
kuhakikisha taarifa za awali zinafikia jamii kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka
kupitia vyombo vyao vya habari.
Pia
imewasisitiza wanahabari kuendelea kuwa mabalozi wazuri kuelezea na kusisitiza
umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zote
za kiuchumi na kimaendeleo.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu
Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Hali ya Hewa
Duniani Dkt Ladislaus Chang’a wakati akifungua warsha maalum ya wanahabari
kuhusu utabiri wa msimu wa mvua za Vuli Oktoba hadi Disemba mwaka huu.
Aidha
Dkt Chang’a amewataka wanahabari kuhakikisha wanatumia fursa za taarifa za hali
ya Hewa zinazotolwa na Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kuzisambaza na jamii
ipate uelewa.
‘Mamlaka imeendelea
kutoa huduma za utabiri wa maeneo madogo kwa wilaya zote za mikoa iliyopo
katika ukanda unaopata mvua za Vuli. Utabiri wa Wilaya 86 umeandaliwa kwa
maeneo husika. Hivyo, natoa wito kwenu wanahabari kuhakikisha kila wilaya na kila
sekta inapata taarifa hizi kwa wakati ili wafanye maamuzi na kuweka mipango ya
kuboresha huduma zao kwa lengo la kuongeza tija na kupunguza madhara ya hali
mbaya ya hewa yanapojitokeza, kwa namna hii itafanya taarifa hizi za utabiri
ziwe na tija iliyokusudiwa’amesema Dkt Chang’a
Dkt Chang’a amesema kuwa Mamlaka imeendelea kutoa utabiri wa misimu mbalimbali pamoja na tahadhari pindi kunapokuwa na matarajio ya hali mbaya ya hewa ili kusaidia wakulima,wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuweza kuchukua tahadhari.
Awali akizungumza
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri TMA Dkt Hamza Kabelwa ametumia fursa hiyo
kuwapongeza wanahabari na kusema nao wamekuwa ni watabiri kutokana na kufahamu
mambo mengi.
‘Hawa wanahabari wote
ni watabiri vilevile kwa hiyo wanaongeza mchango wao katika namna ya kuboresha
na pia wanafahamu maana ya El Nino na La Nina kutokana na namna wamekuwa
wakijifunza mara kwa mara’amesema Dkt Kabelwa
Akizungumza kwa niaba
ya wanahabari Mwandhi Bernard Lugongo kutoka gazeti la Dailynews,amesema taaria
ambazo wamekuwa wakizitoa zimepelekea serikali pamoja na wadau mbalimbali
kuweka mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Hata hivyo Mamlaka hiyo hapo kesho inatarajia kutoa utabiri wa msimu wa Mvua za Vuli kuanzia Oktoba hadi Disemba mwaka huu,hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kufuatilia taarifa sahihi zinazotolewa na Mamlaka hiyo.
Post a Comment