****
Tausi Mbowe
Katika kuhakikisha wafanyabishara wa Dawa na Vifaa Tiba nchini wanawekewa mazingira mazuri ya biashara Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeweka mikakati maalum.
Mkakati huo una lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabishara na wazalishaji wa Bidhaa za Dawa na Vifaa Tiba nchini.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano ya mamlaka hizo wakati wa ziara ya Bodi ya Wizara ya Afya ya TMDA (MAB), ilipofanya ziara na kukutana na Uongozi wa TRA katika Bandari ya Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine ushirikiano huo unalengo la kuondoa vikwazo wanavyokutana navyo wazalishaji wa ndani wa dawa na vifaa tiba wanapoingiza malighafi kutoka nje ya nchi.
Bidhaa hizo ni kama Sukari ambayo hutumika katika uzalishaji ambako TRA inaainisha sukari kana bidhaa iliyokamilika tayari kwa matumizi hivyo inapaswa kulipiwa kodi kama bidhaa nyingine lakini TMDA imehainisha kama malighafi hivyi kuingeza mzigo wa kodi kwa wazalishaji hao.
Ili kuondokana na kadhia hiyo, pande zote mbili zimekubaliana kupitia na kufanya marekebisho ya sera za kodi ili kuleta uelewa wa pamoja ili kuvutia uwekezaji wa ndani.
Mamlaka hizo pia zimekubaliana kuboresha mfumo wa "Electronic Single Window System" kuondoa "HS Codes" za bidhaa ambazo hazohusiki na TMDA ili kurahisisha na kupunguza muda wa kuruhusu bidhaa na zisichukue muda mrefu hivyo kuondoa usumbufu kwa wateja wakati wanapotoa mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.
Hii inadhibitisha dhamira ya TRA na TMDA kuhakikisha wanawasaidia wafanyabiashara na wazalishaji wa ndani wa dawa na vifaa tiba ili waweze kutosheleza soko la ndani na kupunguza uagizaji kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo ameishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa ushirikoano wao hasa katika uboreshaji wa mfumo huo.
Dk Fimbo amesema huduma hiyo imepunguza malalamiko kwa kiwango kikubwa yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyabishara na wazalishaji wa dawa ba vifaa tiba nchini na watoa miIgo wakati waliipokuwa wakiingiza malighafi hizo Bandarini.
Naye Kamishna wa Forodha wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Juma Bakari amesema,
mamlaka hiyo ina dhamira ya dhati ya kuboresha Mfuko wa Umeme wa Kielectronics Single Window.
Kamishna Bakari aliwataka TMDA kuendelea kutoa maoni juu ya mfumo huo kwa kuorodhesha hoja za msingi na kuziwasisha katika mamlala hiyo ili zifanyiwe kazi kwa lengo la kuchochea mazingira mazuri ya biashara nchini na hatimaye kuwe na tija katika pato la Taifa.


Post a Comment