Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro imekusanya zaiidi ya Sh373 bilioni kutokana na mauzo ya zao la Kakao.
Makusanyo hayo yamepatikana katika msimu wa mauzo ya mwaka 2023/2024 pekee.
Akizungumza jana Alhamisi, Agosti 15, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli amesema fedha hizo zimdpatikana kutokana na kutumia Minada kwa njia ya Kiitronic unaondeshwa na Soko la Bidhaa (TMX).
Kwa mujibu wa Judith awali mapato ya halmashauri hiyo yalikuwa chini hadi kufikia Sh39 bilioni kutokana na zao hilo lakini tangu kuanza kwakwa njia ya electronic yamepanda npaka Sh 373 milioni.
" Mvomero tumeingia katika mfumo wa minada kwa miaka mitatu sasa na tumeanza na zao la Kakao lakini tumepata faida kubwa mwaka 2020/2021 wakati tunaanza tulikusanya Sh39 bilioni pekee mwaka 2022/2023 tukafiksha Sh127 milioni na mwkaa huu wa fedha tumefikisha zaidi ya Sh 373 milioni."
Judith alisema kwa upande wa pato la mkulima limeongezeka kutoka Sh1. 3 bilioni mwaka 2020 mpaka kufikia Sh44.7 bilioni kwa msimu huu.
Kwa upade wao wakulima wa zao hilo wameeleza kuridhishwa na usimamizi wa minada ya zao hilo ambayo imeendeshwa kwa njia ya kielektroniki.
Tumaini Kelvin alisema mfumo huo wa TMX umekuwa mkombozi kwani sasa wanapata fedha kwa wakati lakini umeongeza uwazi katika biashara yao kwani wanashuhudia minada inavyofanyika.
Post a Comment