TRC YAOMBA RADHI BAADA YA TREINI YA SGR KUPATA HITILAFU


*****

 Shirika la Reli Tanzania (TRC) limewaomba radhi abiria waliosafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na treni ya kisasa (SGR) jana Alhamisi, Agosti 1, 2024 kutokana na hitilafu iliyojitokeza wakati wa safari hiyo.

Taarifa ya TRC iliyotolewa leo Ijumaa, Agosti 2, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa shirika hilo, Jamila Mbarouk imesema kutokana na hitilafu hiyo treni hiyo ilichelewa kufika jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo taarifa hiyo imeomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2:15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 1, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea eneo la mtaa wa Mshikamano, Kata ya Kihonda mkoani Morogoro.

0/Post a Comment/Comments