NA: Issah Mohamed –Dar es salaam.
EMAIL: issahmohamedtz@gmail.com
Chama cha Tiba Asili na Utafiti wa mitishamba –UMAWATI, kimekemea wimbi la vitendo vya upotevu wa watoto pamoja na wenye ulemavu ambavyo jamii imehusisha vitendo hivyo na imani za kishirikina.
Kauli ya chama hicho kimetolewa na Mkurugenzi wake Dkt Riziki Mkali Malela Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya ujio wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa mzimu wa Afrika ambayo yanatarajiwaa kufanyika katika Kijiji cha kwa masanja, Wilayani Chalinze Mkoani Pwani Septemba 5 hadi 7.
Amesema chama hicho hakikubaliani na tiba zinaoenda sambamba na imani za kishirikina pamoja na kukemea baadhi ya waganga wa asili wanaojihusisha na vitendo hivyo kwani ni kinyume cha mila na destruri za mtanzania.
‘’Kuna imani ambayo ipo ya upoteveu wa watoto ambazo zimehusisha na imani za kishirikina, kwakweli sisi kama UMAWATI hua tumekua mstari wa mbele kukemea hata vitendo dhidi ya wenye ulemavu’’ Amesema Dkt Riziki.
Sambamba na hilo Dkt Malela amewahasa watanzania kurudi katika mtindo wa maisha wa asili ikiwemo ulaji wa vyakula ili kupunguza magonjwa yasioambukiza huku akiwasisitiza wataalam wa tiba asili kujikita katika utoaji elimu.
‘’Mimi nafkiri kama UMAWATI tumejipanga kushirikiana na serikali katika kuelekeza nguvu zetu hasa waganga wa Afrika Mashariki katika kubaini ongezeko la magonjwa Afrika Mashariki’’ Ameongeza Dkr Riziki.
Akizungumzia maadhimisho ya mwaka mmoja wa mzimu wa Afrika Katibu wa –UMAWATI Taifa , Ally Mnyanga amesema kwa kushirikiana na serikali wamekusudia kuimarisha na kukuza tiba za asili katika eneo la Afrika Mashariki.
Aidha maadhimisho ya mzimu wa Afrika yanatarajiwa kuwa na athari chanya katika kukuza tiba za asili na kuimarisha urithi wa kiafrika kwa jamii za Afrika na mashariki na kwingineko.
Post a Comment