Wadau mbalimbali walipotembelea ufugaji wa kisasa unaofanywa na Ayubu Urio na kupata elimu.namna ya ufugaji bora wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa.
...............
Happy Lazaro,Arusha .
Vijana nchini wameshauriwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo.na Mifugo kwani kuna fursa nyingi sana zitakazowasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkulima na Mfugaji wa ng'ombe bora wa maziwa pamoja na kuku ,Ayubu Urio wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha.
Urio amesema kuwa,sekta ya Mifugo na kilimo ni sekta ambayo inachangia pato kubwa kwa Taifa na limekuwa likitoa ajira nyingi sana kwa wananchi wake.
Amefafanua zaidi kuwa,umefika wakati sasa wa vijana kujikita zaidi katika kilimo na ufugaji kwani kinalipa kwa kiwango kikubwa sana na kinatoa fursa za ajira kwa idadi kubwa ya wananchi.
"Nawaomba sana vijana wasiendelee kualamika kuhusu ajira badala yake wachangamkiem fursa zilizopo katika sekta hizo kwani kuna mafanikio makubwa sana kutokana na soko kuendelea kupanuka ndani na nje ya nchi."amesema .
Aidha amesema kuwa amekuwa akifanya ufugaji bora na wa kisasa ambapo kupitia ufugaji wake amekuwa akifundisha wafugaji namna bora ya ufugaji wa kisasa kwa kutumia shamba darasa ambapo wafugaji wamekuwa wakitoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuja kujifunza na kupata elimu zaidi juu ya ufugaji bora "amesema .
Urio ameongeza kuwa ,tangu ameanza kujishughulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa amepata mafanikio makubwa sana na kuweza kuwa mfano bora wa kuigwa kwa wakulima kutoka mkoa wa Arusha na nje ya mkoa wa Arusha .
"Nawakaribisha wafugaji kutoka maeneo mbalimbali kuja kujifunza ufugaji bora wa kisasa na kuweza kufanya ufugaji wenye tija utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi. "amesema .
Post a Comment