Afisa Program Mwandamizi LHRC Raymond Kanegene akizungumza
na waaandishi wa habari katika kikao cha kujadili muendelezo wa Mchakato wa
uandishi wa ripoti ya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ambacho
kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es salaam.
Mwakilishi kutoka Shirika la Save The Children Innocent Estomih akizungumza na waaandishi wa habari katika kikao cha kujadili muendelezo wa Mchakato wa uandishi wa ripooti ya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ambacho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es salaam
Mwanasaikolojia kutoka Shirika la C-SEMA Jenipha
Kalman akizungumza na waaandishi wa
habari katika kikao cha kujadili muendelezo wa Mchakato wa uandishi wa ripoti
ya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ambacho kimefanyika leo kwenye
ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es salaam.
Thabit Juma kutokea Shirika la msaada wa Kisheria na
Haki za Binadamu Zanzibar (ZALHO) Kalman akizungumza na waaandishi wa habari katika
kikao cha kujadili muendelezo wa Mchakato wa uandishi wa ripoti ya tathmini ya
Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ambacho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mbezi
Garden jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya LHI-Tanzania
William Mtwazi akizungumza na waaandishi wa habari katika kikao cha kujadili muendelezo
wa Mchakato wa uandishi wa ripoti ya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR)
ambacho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es salaam


Baadhi ya wadau ambao wameshiriki katika kikao cha kujadili
muendelezo wa Mchakato wa uandishi wa ripoti ya tathmini ya Hali ya Haki za
Binadamu (UPR) ambacho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar
es salaam.
..............................
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa mchakato wa Ripoti Ya Tahmini ya Hali
ya Haki za Binadamu (UPR) utakapokamilika vizuri kwa mapendekezo kufika
serikalini na kwenye Baraza la Haki za Binadamu italeta matokeo chanya kwa
maendeleo.
Hayo yamejiri kufuatia Asasi zisizo za Kiserikali ikiwemo
Shirika la Save The Children,Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu
(LHRC),Mtandao wa watetezi wa haki za bianadamu (THRDC),Taasisi ya ya Sheria na
Ujenzi wa Afya Tanzania na C-SEMA kujadili muendelezo wa Mchakato wa uandishi
wa ripooti ya tahmini ya Hali ya Haki za Binadamu UPR ambao ulianza tangu mwaka
2022.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika kikao
hicho cha wadau za Kiraia Mwakilishi kutoka
Shirika la Save The Children Innocent Estomih amesema kuwa wanategemea
mapendekezo yaliyotolewa yanazingatiwa na kupelekea chachu ya maendeleo.
Afisa Program Mwandamizi LHRC Raymond Kanegene
amesema ni vyema serikali ikashirikana na asasi za kiraia ili kukubaliana kuwa
na mtizamo mmoja zilizona ukweli na uhalisia katika jamii.
Aidha baadhi ya wadau Mwanasaikolojia kutoka Shirika
la C-SEMA Jenipha Kalman,Thabit Juma kutokea Shirika la msaada wa Kisheria na
Haki za Binadamu Zanzibar (ZALHO),pamoja
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya LHI-Tanzania William Mtwazi wamesema
wanatumaini mapendekezo waliyoyatoa kwenye ripoti hiyo zitakwenda kutatuliwa.
Mchakato wa uandishi wa ripooti ya tahmini ya Hali
ya Haki za Binadamu UPR ambao ulianza tangu mwaka 2022 ambapo serikali
ilifanyiwa tathimini na Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Umoja wa Mataifa la
Haki za biandamu,Jumla ya Mapendekezo 252 yalitolewa na Tanzania ilikubali
mapendekezo 187 ili kufanyia utekelezaji kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka
2022/26
Post a Comment