Na Damari Tandasi
AFISA Mwandamizi Kodi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Philipo Eliamini amewaasa wananchi wote wanaotembelea maonesho ya wakulima na wafugaji (88) kufika katika banda lao ili waweze kupata elimu kuhusiana na masuala ya kodi pamoja shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya 88 Nzuguni jijini Dodoma,Waliamini amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwao kuonana na wananchi kuwapa elimu ikiwemo ya masuala ya kokodi,masuala ya usimamizi wa kodi lakini pia inapokea maoni na malalamiko ya wananchi ambayo pia kuwawezesha kuboresha utendaji wao wa kila siku.
"Kwa hiyo tunasema maonesho haya ni fursa nzuri kwa wananchi kujifunza lakini pia ni fursa nzuri kwetu ambapo tunaweza kuonana na wadau wetu na tunawapa elimu ambayo itawasaidia katika shughuli zao."amesema Eliamini
Ameongeza kuwa "kama mnavyofahamu wadau wa maonesho haya ni wakulima na tunasema kilimo ni biashara,lakini tunafahamu serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa sana kwenye masuala ya kilimo lakini pia inatoa misamaha mbalimbali kwenye eneo la kilimo matarajio ni kwamba wakulima hawa wanapofanya shuguli hizo na kupata kipato kitakachofikia kiwango cha kutozwa kodi basi na wao waweze kuichangia serikali katika masuala mazima ya kodi"
Amesema kila mwaka serikali kupitia Bunge inafanya mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo sheria za kodi na kwamba , kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 kumefanyika mabadiliko mbalimbali ya kikodi na kwa upande wa sheria za kodi kuna misamaha mbalimbali ya kodi ambayo inaenda kuleta unafuu mkubwa kwa wakulima.
Amesema wanawaomba wakulima waweze kutembelea banda la TRA ili waweze kupate elimu ya misamaha ya kodi ambayo imepitishwa na bunge ili waweze kupata elimu hiyo na kujua zana ambazo zimesamehewa kodi.
Pia wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo namba ya utambulisho wa mlipa kodi
Kama mnavyofahamu mabadiliko ya sheria ya mwaka jana yaliweka kipengele cha kila raia kuanzia miaka 18 na kuendelea anapaswa kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi
Pia wanatia namba ya utambulisho wa mlipa kodi kikubwa mtu awe na nbamba ya nida
Pia wanatoa huduma ya makadirio ya kodi kwa mfanyabiashara ambaye bado hajakadiriwa makadirio ya kodi kwa mwaka huu wa fedha
Wanaodaiwa kodi na wanahitaji kupata namba za malipo vile vile huduma hiyo inapatikana katika banda hilo
Pia wapo na wasambazaji wa mashine za kutolea risiti za EFD na zile za VFD,wanatoa elimu ya matumizi ya mashine hizo na wataalam wapo na mashine zipo kwa wanaohitaji kununua
Kila mfanyabiashara mwenye mauzo ya kuanzia shilingi milioni 11 kwa mwaka anapaswa kununua na kutumia mashine hizo
Katika maonesho hayo wanapata fursa nzuri ya kujenga mahusiano mazuri na wadau ambao ni walipa kodi na kupata maoni,malalamiko ambayo yataisaidia TRA kuendesha ahughuki zao za kiutendaji huku akisema hata mabadiliko yanayofanyika ni kutokana na maoni ya wadau mbalimbali.
Post a Comment