WATENDAJI UDART MATATANI KWA KUFANYA MAKUBALIANO BATILI

******

Na Mwandishi wetu


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Temeke imebaini  kuwa baadhi ya watumishi wa wakala wa mabasi yaendao kasi UDART waliingia makubaliano batili na watendaji wa kampuni iitwayo Sahara African Beauty kwa ajili ya kujenga jengo la kudumu lenye vyumba sitini kinyume na sheria ya barabarani namba 13/2007.                                                                 

Akizungunza na waandishi wa habari jijini Dar es salaamu leo Agosti 2,2024 juu ya tathimini ya utendaji katika kipindi cha miezi mitatu mkuu  wa Takukuru  mkoa wa Temeke Holle Makungu, amesema uchunguzi waliofanya umebaini ujenzi huo umefanyika bila hata kibali cha mkurugenzi wa wa manispaa ya Temeke kinyume cha kanuni ya 124(1) inayozuia kufanyika kwa ujenzi bila kibali cha Mamlaka za serikali za mtaa kwa eneo husika 

Hata hivyo Takukuru imesema  imejirizisha kuwa hifadhi za barabara zote nchini zipo chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa mujibu wa sheria 

Aidha Takukukuru Temeke  imebaini dosari katika miradi miwili kati ya miradi 10 iliyo fanyiwa uchunguzi ndani ya miezi mitatu huku pia mifumo 7 ya uchambuzi nayo ikibainika kuwa na mianya ya rushwa hali iliyo ifanya taasisi hiyo kuitaka Halmashauri kufanyia kazi dosari hizo.

Amesema licha ya kubaini dosari na mianya hiyo wametoa ushauri wa kufanyiwa kazi kwa dosari hizo ili kuepusha upotevu wa mapato katika miradi ya maendeleo pa moja na mifumo ya uchambuzi.





 

0/Post a Comment/Comments