WIZARA YA FEDHA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

Afisa Msimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mzava, akizungumza wakati wa semina ya utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa Wilaya ya Mtama mkoani Lindi, ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo uwekezaji, mikopo na akiba.

Afisa Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Bw. Adolf Ndunguru, akigawa vipeperushi vyenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo, akiba uwekezaji kwa baadhi ya wananchi wa Wilaya vya Mtama mkoani Lindi, waliojitokeza kupata elimu ya masuala ya fedha.
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhan Myonga, akieleza umuhimu wa kusoma mikataba kabla ya kuchukua mikopo kwa wananchi wa Wilaya vya Mtama mkoani Lindi,waliojitokeza kupata elimu ya masuala ya fedha.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bi Aveline Kapologwe akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mtama mkoani Lindi waliofika kupata elimu ya fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwepo masuala ya mikopo, kujiwekea akiba na masuala ya uwekezaji.
......................

Na. Josephine Majula, WF, Lindi 

Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha nchini, inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo Wahamasishaji wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha, Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha, Watoa Huduma za Fedha, Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Mahitaji Maalum.

Lengo la kutoa elimu hiyo  ni kuhakikisha inaongeza idadi  kubwa ya watu wenye uelewa mpana wa  masuala ya fedha na kupata maarifa juu ya upatikanaji na utumiaji wa huduma rasmi za kifedha.

Wizara ya Fedha inaendelea kuwasisitiza Wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapobaini kuwepo wa Mtoa Huduma asiyesajiliwa au anayetoa huduma za fedha hizo kinyume cha Sheria na utaratibu uliowekwa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

0/Post a Comment/Comments