*******
Na Mwandishi wetu
TAASISI inayojishughulisha na masuala ya Mazingira 'Environmental Conserarvation Community of Tanzania (ECCT) imeitaka Jamii kuweka kipaumbele Cha utoaji elimu kwa watoto na vijana mashuleni juu ya masuala ya utunzaji wa mazingira kwa lengo la vizazi endelevu vinavyothamini umuhimu wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi hiyo Lucky Michael mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam wakati akitoka elimu ya Ulegerezaji taka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Daniel Chongolo kama sehemu ya Taasisi hiyo Kuadhimisha siku ya usafi wa Mazingira Duniani.
Akizungumzia hatua hiyo Lucky alisema kuna umuhimu mkubwa kwa kizazi cha watoto hususani waliopo shuleni kupewa elimu hiyo itakayowasaidia kuwajengea kiakili na kifikra katika suala zima la utunzaji mazingira kuanzia wakiwa na umri mdogo hali itakayowawezesha kuwa na uelewa mpana wa suala hilo.
"Wakati huu ambao Taifa letu Tanzania tunaendelea kupiga hatua kubwa katika utunzaji wa mazingira, sisi kama jamii tuna kila sababu ya kukielimisha kizazi cha watoto wetu walioko shuleni ili kukiwezesha kutambua faida za mazingira wakiwa bado wadogo" alisema Lucky.
Aidha kwa upande wake Afisa Habari wa ECCT Nyanzobe Makwaia pamoja na hilo alisema katika kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utunzaji wa mazingira, mbali na utoaji wa elimu kwa watoto mashuleni ,taasisi hiyo pia imekuwa ikishiriki moja kwa usafi wa mazingira ikiwemo maeneo ya fukwe za Bahari na kwingineko.
Pamoja na hilo alisema taasisi ya ECCT iliyonzishwa miaka minne iliyopita kwa kiasi kikubwa imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kutimiza malengo yake ya utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu za utoaji wa huduma za jamii.
Aidha kwa upande wake Mwalimu wa Mazingira wa Shule ya Daniel Chongolo Mwanahamic Mhando mbali na kushukuru ECCT kwa kutoa elimu shuleni hapo alisema, kwao jambo hilo lilikuwa ni takwa kubwa kutokana na upya wa Shule yao.
Alisema kutokana na uchanga wa Shule hiyo kwa kiasi walikuwa na uhitaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kwa lengo la kuifanya Shule hiyo kuwa na mandhari ya kuvutia ikizingiatiwa kuwa Shule hiyo ipo maeneo ya karibu na bahari hivyo uhitaji wa elimu ya mazingira kuwa ni suala muhimu kwao.
Nao raia kutoka Korea Min Jeong Lee na Minj Kim ambao wapo wapo nchini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kuhusu utunzaji wa mazingira kupitia taasisi hya ECCT, wameipongeza Tanzania kutokana na juhudi inazozichukua kuboresha mazingira.
Wamesema uwepo wao hapa nchini ni jambo linalowapa faraja huku wakiamini juhudi hizo zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau kutoka sekta Binafsi katika nyanja ya mazingira itazidi kujiweka juu Tanzania kimazingira.
Ends
Post a Comment