Mama wa hayati Steven Kanumba Ni miongoni mwa wageni wanaohudhuria tamasha la Faraja ya Tasnia ambalo linalenga kuwaenzi wasanii na wanatasnia wote waliotangulia Mbele za haki.
Mama Kanumba amewaambia waandishi kuwa walioofikiria kuja na tamasha hilo wamefanya jambo jema kwani kuwaenzi wasanii na wengine walio kwenye tasnia ni moja ya njia ya kuonesha kuwa watu hao bado wanathamini wa jamii.
Mama kanumba Amesema kuwa Leo ni siku ya faraja kwani Bado anamkumbuka mwanae mpaka Leo”Leo ni siku muhimu kwangu kabla ya kuja hapa nilivyoamka nililia sana namkumbuka mwanangu”.Amesema mama kanumba
Tamasha la Faraja ya Tasnia limeandaliwa na msanii Steve Nyerere na linafanyika katika uwanja wa Leaders Club,Kinondoni.
Miongoni mwa wanatasnia wanaoenziwa kwenye tamasha hilo Ni pamoja na Marehemu Steven Kanumba,Albert MaNgwair,Amina Chifupa,Mzee Matata,James Dandu(mtoto wa Dandu),Ruge Mutahaba,Mzee Majuto,Sajuki,Godzilla,Sharon Milionea,Kibonde,Mandojo,Gardner G Habash,Remi Ongala,Maunda Zorro,Captain Komba,Bi Kidude,na wengine
Post a Comment