RAIS SAMIA ZIARANI JAMUHURI YA WATU WA CHINA

..............

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Watu wa China. 

Ziara hiyo inatarajiwa kuanzia leo Jumatatu Septemba 02,2024  hadi 06 Septemba ambako  atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC) utakaofanyika jijini Beijing. 

Wakati wa ziara hiyo Rais Samia atakutana na mwenyeji wake Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China kwa mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano muri na wa kihistoria kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China ulioasisiwa miaka 60 iliyopita.




 

0/Post a Comment/Comments