Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) Abdallah Ally Pendekezi wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Uhifadhi shirikishi wa mikoko na Bionuwai zilizopo Delta ya Rufiji ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Salum Maganya akifuatilia kwa makini wakati alipozindua wa mradi wa Uhifadhi shirikishi wa mikoko na Bionuwai zilizopo Delta ya Rufiji ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi wa Taasisi ya Pakaya Culture Environmental Groups Bakari Hassan Kisoma akielezea utekelezaji wa mradi wa Delta ya Rufiji kwenye uzinduzi wa mradi wa Uhifadhi shirikishi wa mikoko na Bionuwai zilizopo Delta ya Rufiji ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Baadhi ya wadau ambao wameshiriki katika kwenye uzinduzi wa mradi wa Uhifadhi shirikishi wa mikoko na Bionuwai zilizopo Delta ya Rufiji ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
.............................
NA MUSSA KHALID, KIBITI PWANI
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) limewataka watanzania kuendelea kupigania uhifadhi wa mazingira Ili kuondokana na changamoto zinazotokana na uharibifu wake.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika Hilo Abdallah Ally Pendekezi wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Uhifadhi shirikishi wa mikoko na Bionuwai zilizopo Delta ya Rufiji ambao umefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Aidha Pendekezi amesema kuwa uzinduzi huo unalenga kutekeleza mradi unaohusiana uhifadhi wa mazingira kwa kwenda kutekeleza upandaji wa mikoko lakini kutengeneza vituo vidogo vya masuala ya utalii vitakavyowawezesha wananchi kujipatia kipato.
‘Makusudio yetu ni kwaajili ya kuwaondoa masikini katika umaskini na kuwaleta kwenye ahueni ya maisha kwa kutumia rasilimali mbalimbali zinazopatikana katika mazingira hayohayo wanayoishi’amesema Pendekezi
Awali akizindua mradi huo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Salum Maganya amewapongeza PAKAYA kwa kunyesha mchango wao katika utunzaji wa mazingira jambo linalosaidia utunzaji wa Mazingira.
Ametoa rai kuhakikisha mashirika hayo yanapofanya utekelezaji wa utunzani wa mazingira yanawashirikisha watu wa chini ili wajue nini kifanyika kwenye maeneo yao jambo litakalokuwa limefanywa kwa faida
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi wa Taasisi ya Pakaya Culture Environmental Groups Bakari Hassan Kisoma amesema mradi huo unafanyika katika kata sita ikiwemo ya Msala,Kiongoroni,Mbuchi,Maparoni,Salale na Mwambao ambapo watahikisha wanapanda mikoko katika maeneo ambayo yameathirika.
Amesema pia wataanzisha na uendelezaji wa wafugaji wa Nyuki kwa baadhi ya vijiji lakini pia kuanzisha vituo vidogo vidogo vya biashara kwa ajili ya bidhaa za bahari na mazao yake na Pwani kwa ujumla.
‘Hii itarahisisha kuondoa uvunaji holela wa mikoko ambapo watu wanakwenda usiku na mashua zao na kuikata hivyo kukiwa na vituo rasmi hizo bidhaa zitakuwa zinatangazwa pale na watu wa TRA watakwenda kuchukua ushuru wao huku na TFS nao taratibu zao watazifanya vizuri’amesema Kisoma
Ameendelea kusema kuwa utalii wa kiutamaduni watakapokuwa wameanza na kutangaza kwa kiasi cha chini kwa mwaka watakuwa wameongeza mapato makubwa.
Shirika la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) lilianzishwa mwaka 2006 kwa lengo la kufanya utetezi pamoja na kushirikisha wananchi kwa ajili ya kupigania uhifadhi wa mazingira pamoja na uenezaji wa elimu ya mazingira.
Post a Comment