Na Tausi Mbowe
Mamlaka ya Chakula ya Indonesia pamoja na Mamalaka. ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), zimeingia makubaliano ya kushirikiana katika Udhibiti.
Mkubaliano hayo yamefanyika leo Septemba 3, 2024 katika Kongamano la pili la nchi za Indonesia na Afrika .
Kongamano hilo la siku tatu limeanza Septemba Mosi mpaka tatu nchini Indonesia.
Hati ya makubaliano hayo (MoU), ilisainiwa mnele ya viongozi wa pande zote mbili ambapo pamoja na mambo mengine taasisi hizo zenye jukumu la kusimamia masuala yote ya Chakula, Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi zitashirikiana ili kuboresha sekta ya afya katika nchi zao.
Mamalaka ya Dawa, na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), inajukumu la kulinda afya ya mlaji katika usimamizi na udhibiti wa Dawa, Vifaa Tiba na Vijtendanishi.



Post a Comment