Vijana wa Mkoa wa Dar Es Salaam hatupotayari kutumika kuhatarisha amani ya Nchi yetu kwaajili ya watu wachache ambao hawaitakii mema nchi yetu kwa kulinda maslahi yao binafsi.
Hayo yamezungumzwa na vijana wa taasisi ya jamii mpya katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar Es Salaam,akizungumza kwa niaba ya vijana wa Wilaya ya Temeke Donatila Thomas nakusema kuwa hao watu wana maslahi yao binafsi hivyo vijana hawapo tayari kuingia katika mtego wao.
Pia mwakilishi kutoka Wilaya ya Ubungo Kija amesema kipimo na viashiria vya amani ni shughuli za maendeleo hasa ya kisiasa na uchumi hivyo watakapo acha kufanya kazi na kuingia barabarani hakutasaidia katika kukuza pato la Taifa na hata wao pia watakuwa wamepoteza muda ambao wangeutumia vizuri katika kutafuta pesa kuweza kujikimu na kuendesha maisha yao.
Post a Comment